Msururu wa PTE Kiswahili

Front Cover
East African Publishers - Swahili language - 256 pages
2 Reviews
 

What people are saying - Write a review

User Review - Flag as inappropriate

hi ni kazi mufti ambayo mwandishi ameandika. amerahisisha kazi yetu sisi walimu wa shule za msingi
.EMILY MUCHIRA

User Review - Flag as inappropriate

Chapisho hili ni kanzi kwa mwanafunzi-mwalimu na mwalimu wa Chuo chochote kile cha Ualimu Afrika Mashariki anayesomea au kufundisha taaluma ya ualimu. Mwandishi ametanguliza shabaha za kufundisha Kiswahili Kitaifa. Sura ya kwanza imejadili kwa kina fasili ya lugha, historia yake katika jamii ya Wayunani, Fasili ya Isimu, sifa-bia za lugha na misingi ya uainishaji wa lugha na umuhimu wa lugha. Sura ya pili imetathmini kwa uketo swala la Isimu-jamii kuhusu sajili/rejesta katika mawanda ya dini, sheria, sayansi na teknolojia, biashara, magazeti na michezo. Maelezo yameambatana na michoro ili kuifafanua dhana kwa undani wake. Sura ya tatu inachunguza Historia ya Kiswahili. Mwandishi amehakiki nadharia mbili zinazodai kuwa Kiswahili ni lugha mseto na nadharia ya pili inayoshikilia kuwa Kiswahili ni zao la Wabantu. Tahakiki hii imetathmini mihimili na upungufu wa kila nadharia kabla ya kuhitimisha mjadala. Katika sura ya nne mwandishi amefafanua matayarisho muhimu yanayohitajika kufanywa kabla ya zoezi la ufundishaji. Aidha ameeleza umuhimu wa vifaa vya kufundishia kama vile: Ratiba ya mafunzo, Andao la somo, Hifadhi ya kazi na Kumbukumbu za tathmini. Sura ya tano imezingatia kiwango msingi cha isimu ambacho ni Fonetiki. Lengo la kufanya hivyo ni kuainisha fonimu za Kiswahili na kuonesha utamkaji wake sahihi. Mwandishi amezigawa kwenye makundi mawili yaani Irabu na Konsonanti. Sura ya sita imezingatia stadi ya kusikiliza na kuongea. Mwandishi ametoa mwelekeo bayana wa kufundisha stadi hii kwa makini huku akichambua kwa kina mbinu mbalimbali za kuandaa somo na kulifundisha. Sura ya saba imezingatia stadi ya Kusoma. Vitabu vingi vilivyochapishwa havitilii maanani stadi hii. Hii ndiyo sababu ya mwandishi kuizingatia upekee wake katika maelezo yake zamifu. Sura ya nane imetalii mawanda ya fasihi andishi na ufundishaji wake. kwenye sehemu hii amezingatia ufundishaji wa kazi nathari na zile za ushairi. Hata hivyo mwandishi hakugusia kipengele muhimu cha fasihi simulizi. Kwenye sura ya tisa mwandishi amezama katika ufundishaji wa sarufi. Kwa hakika sehemu hii imeondoa utata wa uainishaji wa kategoria za maneno na pia ngeli za Kiswahili. Kwa ufasaha mkuu na umakini mwandishi ameainisha kategoria zifuatazo za maneno: Nomino, Vivumishi, Vitenzi, Vielezi, Vihusishi, Vihisishi na Viwakilishi na aina zake. Utaratibu anaouzingatia kuainisha ngeli ni ule wa kimofolojia unaozingatia upatanisho wa kisarufi.Sura za mwisho zinatoa maswali ya tathmini na majibu yake. Alex Umbima Kevogo 

Contents

Sajili za Lugha
7
Historia Fupi ya Kiswahili
13
Matayarisho ya kufundisha
25
Fonetiki
38
Kusikiliza na Kuongea
44
Kusoma
58
Fasihi Andishi
89
Sarufi
98
Msamiati
147
Maswali ya Marudio
179
Majibu
214
Copyright

Bibliographic information